Somo la 1
Tunayo habari njema. Kwamba Mungu ameahidi kutupenda na kutusamehe, huku akitupatia uzima ambao hauna mwisho, uhuru wa kuacha uovu, na kupata urafiki wa karibu naye kwa kadiri tunavyomtegemea na kumtii katika upendo.
Je, unaliamini hilo? Je, Unaelewa maana yake?
Biblia inasema kuwa tulizaliwa ili tuwe na upendo, utii na kumfurahia Mungu milele ingawa tunashindwa.
Kwanini?
Kwasababu tulizaliwa katika uasi kwa njia mbili:
Kwanza, hatumjui, na hatuwezi kumpenda fulani tusiye mfahamu!
Pili, tumezaliwa katika hali ya uovu ambayo imetutenganisha na uzima, ufahamu, na upendo wa Mungu. Tamaa yetu ya maovu imetusababishia kifo, magonjwa, kukosa haki, vita na maisha ya huzuni.
Je, tamaa ya uovu imetutenga na Mungu kwa namna gani?
Hali ya uovu ni ubinafsi ambao unatuletea mateso katika mahusiano. Kadri mume anavyo kuwa karibu na mke wake ndivyo anavyotambua kuwa maneno yake, matendo, na fikra zake zinaweza kumkwaza. Ndivyo ilivyo katika ushirikiano wetu na Mungu. Kadri tunavyomkaribia Mungu ndivyo tunaelewa jinsi uovu wetu unavyotutenga naye.
Je ni lipi lilikuwa jibu la Mungu kuhusu kujitenga kwetu na kumuacha?
Mungu aliamua kufanyika kuwa mwanadamu ili kuurudisha urafiki wetu na yeye. Mwanadamu huyo alikuwa ni Yesu.
Je, ni muhimu kiasi gani kwa Mungu kufanyika kuwa Mwanadamu?
Kwanza, alitaka kuhusiana nasi kibinafsi. Pili, alitaka kupata uzoefu wa furaha yetu, maumivu, na mateso yetu. Tatu, alitaka kubeba adhabu kwasababu ya maovu yetu kwa kutufia. Na nne, alitaka kufufuka kwaajili ya kutuosha maovu yetu, ili kuturudisha kwake na kutupatia uhai usio na mwisho.
Yesu aliamua kutufia ili atuhakikishie kuwa Mungu anauhukumu uovu. Hatutaki kuwa na Mungu asiyeadhibu uovu. Kifo Cha Yesu ni hakikisho kuwa Mungu hatauacha hivyo uovu. Ndiyo sababu alijipa adhabu kwaajili ya maovu yetu, ingawa yeye hakuwa na kosa lolote.
Kusudi kubwa alilokuwa nalo ni kutupatia uhuru dhidi ya tamaa za maovu na kuibadirisha mioyo yetu ili tufanyike kuwa rafiki zake. Hivi ndivyo Biblia inavyotuambia kuwa. "Kuzaliwa mara ya pili" humaanisha mabadiriko kamili, na kuishi kwa uhuru pasipo na utumwa wa tamaa za maovu. Ili tuwe na mahusiano na ukaribu na Mungu.
Maana ya habari njema haiishii kwa Yesu kubeba adhabu yetu.
Biblia inasema kuwa baada ya Yesu kufa, alifufuka na sasa anaishi. Anatupatia Maisha mapya. Maisha makamilifu ambayo yasiovunjika. Tunapokea zawadi ya ajabu, na Roho wake anaweza kuishi ndani yetu na kuzibadili polepole tamaa zetu za maovu, ili tuzae hisia zetu katika utakatifu.
Matoleo ya kusafishwa na kufanywa wakamilifu yanaitwa "Utakaso". Sisi hatutakuwa wakamilifu mpaka tutakapoondoka katika maisha ya dunia hii. Ingawa kwa matokeo hayo tunaweza kujaribu kwa sasa.
Matokeo hayo yanaitwa Tunda la Roho, ambalo ni: Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Utu Wema, fadhili, Uaminifu, Upole, na Kiasi. Tutaonyesha kuwa sisi ni Wakristo tutakapokuwa na tabia hizi. Kama hatuna Kristo huu ndio wakati wa kujisalimisha kwa Mungu na kumsogelea zaidi kwa kujisomea Biblia, kugeuka kutoka maovuni, kuomba, na kumwabudu yeye.
Hatuwezi kukuza tunda la Roho. Ni Roho tu anayeweza kutukuza kwa kadri tunavyoonyesha upendo wetu kwa Kristo.
Biblia inatuambia kuwa inatupasa kuubeba msalaba wetu na kumfuata Yesu. Hiyo ndiyo ishara ya kufa kwa ubinafsi wetu. Kama Yesu alivyobeba msalaba wake (chombo Cha mateso) hadi akafa akiwa ametundikwa juu yake, nasi ndivyo tunapaswa kuonyesha alama ya kufa kwa ubinafsi wetu.
Je, ni kwanini jambo hili ni muhimu? Kwasababu utu wetu wa kale uko vitani dhidi ya mapenzi ya Mungu. Yesu anahitaji tujitoe kabisa na kumtegemea. Anatutaka tubadili shauku zetu za ubinafsi kwa njia ya shauku ya Mungu. Hiyo ni njia ya kuonyesha upendo wetu na utumishi wa unyenyekevu wetu kwa Mungu na kwa watu wake.
Tunapojitoa na kumfanya Mungu awe kiini cha utoshelevu wetu, anatupatia nguvu na shauku ya kumtii. Hapo ni kama tunafanya kumruhusu awe kama pumzi tunayoivuta. Tunamvuta Yesu aingie ndani. Na tunamvuta Yesu aje nje. Jambo hilo linajirudia kila siku mpaka siku ya kufa kwetu. Hili linatutia moyo kumtegemea hata anapotuamuru kuwatendea upendo maadui zetu, na atatusaidia kufanya hivyo.
Ushirika wetu na Yesu ni wa karibu sana na tunapata uzoefu wake. Kwakua Roho wake yuko ndani yetu. Ushirika huu unabadirisha maisha yako kadri unavyomtegemea na kumtii katika upendo. Naye atakusaidia kumheshimu Mungu hata pale unapofanya makosa.
Unaweza kushangaa namna maisha haya yanavyokukosesha furaha kwaajili ya Maisha ya kawaida. Ni furaha sana kukujulisha kuwa upendo na utii wako kwa Mungu utakupatia kuifurahia amani ya Mungu na kupata furaha ya maisha haya.
Ingawa hatujawa huru kikamilifu na tuna hali ya kutamani maovu, tukiendelea kufanya makosa; upendo wetu kwaajili ya Mungu unatupatia njaa inayopunguza nguvu ya mawazo maovu. Mungu anafanya hivyo ili tupate uhuru wa kumfurahia yeye, ulimwengu huu pamoja na mahusiano matakatifu aliyotupatia.
Wengi huona ugumu kuamini ahadi ya Mungu kwamba anabadilisha Matamanio yetu. Ndiyo anafanya hivyo. Hili ni jambo halisi, na kama sivyo, habari njema isingefaa kuwa habari njema.
Kwa nini Wakristo wengi hawaishi maisha mapya?
Kila Mkristo anaweza kuishi huru kabisa mbali na matamanio maovu, lakini kuna nyakati tunapokataa jambo hili. Mara kwa mara tunachagua uovu badala ya Yesu, na hili linatokea hata baada ya kufanyika kuwa Wakristo.
Baadhi wanashindwa kupata uzoefu na uhuru wa kuacha maovu kwasababu hawaamini kuwa hilo linawezekana na hawana uhakika wa kwamba Mungu anawapatia uhuru huo. Wengine hukataa kuishi katika uhuru huo kwasababu una gharama yake. Inawalazimu kujikana kwa ajili ya Mungu.
Hili lina maana gani?
Baada ya kujikabidhi, Mungu anatuagiza kuendelea kujikabidhi. Hili ni jambo endelevu kwasababu mara nyingi tuna mwelekeo wa kuurudia ubinafsi wetu. Biblia inauita mwelekeo huo dhambi ya asili. Hali hiyo tunakuwa nayo tangu kuzaliwa hadi siku ya kufa.
Kadri tunavyo endelea kumwamini na kumtegemea, kuachana na maovu, kuomba, kusoma Biblia, na kushirikiana na Wakristo wengine katika jamii, Roho wa Kristo aishiye ndani yetu huanza kuyabadilisha matamanio yetu na kutupatia uhuru wa kuiacha asili endelevu ya dhambi.
Ukuaji ni swala la muda mrefu. Hupaswi kukata tamaa katika hali hii ya kuendelea kukua na usiitumie hali hii ya kukua polepole kama kisingizio cha kutokukua kabisa.
Kumheshimu Mungu ni chimbuko la furaha ya milele katika ulimwengu huu na isiyoelezeka. Siyo rahisi kuachana na uovu kwa kuwa ni mbaya, ila utoshelevu wa Mungu unatuwezesha kuuacha uovu.
Mungu anatuita tujiunge naye katika utumishi wake uliotukuka. Baada ya kujikabidhi kwake anatuvuvia nguvu ya kuwashirikisha wengine juu ya urafiki huu mzuri sana na hili linaitwa Uinjilisti, na pamoja na kuwafundisha wengine. Ili nao waupate uzoefu huo na Hilo linaitwa Uanafunzi.
Kile anachotupatia Mungu ni kizuri sana kiasi kwamba tukiisha kizoea hatuwezi kuacha kuwashirikisha na wengine. Mara tunapouonja na kuuona wema wa Bwana, tutahitaji kuwaambia wengine ili nao wapate kuihisi furaha ambayo tumepewa.
Tena kuna habari njema (Habari njema zaidi). Mungu anatuahidi upendo na msamaha, maisha yasiyo na mwisho, uhuru wa kuacha maovu, na kuwa rafiki yake wa karibu kwa kadri tunavyomtegemea kwa upendo. Ikiwa tutakuwa waaminifu hadi mwisho wa maisha yetu, anatuahidi miili mipya yenye Utukufu na kuishi pamoja naye milele pasipo na laana ya kuwa watumwa wa maovu, kifo, na kukata tamaa.
Habari mbaya ni kwamba, kila MTU anayekataa zawadi ya Mungu atateseka katika adhabu isiyo na mwisho na kutengwa na Mungu alietupata sote kutoka katika maovu.
Habari njema hugeuka kuwa habari mbaya pale tunaposhindwa kuifanya Injili kuwa jambo la thamani katika maisha yetu.
Tupo ili tumtukuze na kumfurahia Mungu milele. Mara kwa mara tunafikiria kujipendeza wenyewe kuliko kumpendeza Mungu. Ukweli ni kwamba kujiingiza katika tamaa za maovu hazitatufurahisha kwa muda mrefu. Kujihusisha na uovu huleta huzuni, mawazo ya kutojithamini, na kuongeza uovu na tabia mbaya. Uovu unatutawala na kutunyang'anya furaha yetu na pia unatuacha tunajiskia watupu, wapweke na kama watumwa.
Tunapojichunguza wenyewe na kuwa watumishi wenye mapenzi mema kwa wema wa Mungu katika maisha yetu na karama kuu alizotuahidi katika Injili, tunapatiwa uhuru usiopotea.
Hili linachukua kila kitu. Kutii kwetu kuhusu msamaha wake mkuu, maisha na ukarimu wa upendo wake.
Njia rahisi ya kukumbuka jambo hilo ni kupitia Shairi hili la Wokovu:
Yesu, ulikufa msalabani
Ukafufuka kwa walopotea
Nisamehe dhambi zangu zote
Njoo uwe mwokozi wangu Bwana na rafiki
Badili maisha yangu yafanye upya
Nisaidie Bwana, nikuishie
Chimbua Kwa Kina
Soma Yohana ya sura ya 17 ambayo ni kumbukumbu ya maombi aliyoomba Yesu, kwaajili yako na mimi moja kwa moja. Jaribu kuandika yaliyokuvutia juu ya kile alichosema Yesu, kisha soma na kujadiri pamoja na Mkristo mwingine. Unajisikiaje kwamba Yesu alikuombea wewe binafsi?