Lugha

Video ya Somo la 4

Somo la 4

Tulipozungumza juu ya kile ambacho Yesu alitimiza kwa kifo chake, tuliona kwamba kuamini madai yake juu yake mwenyewe kunatupa fursa ya kupata ahadi zake, lakini ili ahadi zake ziwe halisi katika maisha yetu, tunahitaji pia mabadiliko katika mtazamo na tabia.

Mabadiliko huanza kwa kusoma na kuamini kile anachosema kuhusiana na yeye mwenyewe, na kile anachosema kutuhusu sisi. Hapa kuna mifano fulani ya yale ambayo Yesu anasema juu yake mwenyewe tofauti na yale anayosema kutuhusu.

  1. Yesu ni mwema kabisa. Tumejawa na uovu.
  2. Yesu alitupenda. Tulimchukia.
  3. Yesu alituchagua. Tulimkataa.
  4. Yesu alimtii Mungu kikamilifu. Tuliasi dhidi ya kanuni za Mungu.
  5. Yesu aliteseka kwa hiari kwa ajili ya adui zake, ikiwa ni pamoja na sisi wenyewe. Hatukuwa tayari kuteseka hata kwa ajili ya wapendwa wetu.
  6. Yesu alikuwa mtumishi mkuu. Hatutaki kutumikia wengine bali kuhudumiwa.
  7. Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Tumekusudiwa kuanguka katika makaburi yetu, lakini tuna tumaini kwa sababu Yesu anatupa maisha yake.

Yesu ni Mungu, lakini bado yeye ni mwanadamu kamili. Yeye ndiye mtu mkuu zaidi aliyepata kuishi, naye aliamua kutupenda na kufuatilia upendo wetu tulipokuwa adui zake.

Hakuna anayeweza kubadilishwa na Yesu bila kumkaribia kwa unyenyekevu. Yesu sio mchawi. Yeye ni mtu anayejua kila wazo katika akili zetu.

Biblia inasema Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa neema wanyenyekevu. Tukimwendea Yesu tukitaka kumtumia ili tu kujipatia matakwa yetu, kamwe hatutakaribishwa kwake. Kama hatutaacha uovu wetu na kuanza kuuchukia, na kuchagua wema Wake hatutamjua kamwe, wala kupata faida ya ahadi zake.

Mtazamo huu wa kujuta juu ya uovu, pamoja na hamu ya shauku ya wema wa Yesu; na imani thabiti katika ahadi zake; inakuwa kawaida yetu mpya. Tunaposoma yale anayosema katika Biblia, kisha kusali na kutafuta mapenzi yake, mitazamo yetu inabadilika kutoka kwa kiburi hadi unyenyekevu. Tunaanza kuwa kama yeye.

Yesu anaona mioyo yetu. Tunahitaji kukua na kuchukia uovu, na kutamani wema Wake kuchukua mahali pa uovu. Tumuombe Yesu atusamehe, na atatusamehe.

Tunapomkaribia kwa unyenyekevu wa kweli, yeye hukutana nasi katika kuvunjika kwetu na kuanza kurekebisha mioyo yetu. Ni wakati tunapojitazama kihalisi na kuishi kwa bakubaliano ya ukweli ya kwamba Mungu amechagua kutupenda na kutu kuza ndani ya wema Wake, ndipo Mungu hutupatia uhai, furaha, na upendo.

Je, si jambo jema kuona namna anavyo tuhusisha katika mchakato huo?

Ikiwa unaona aibu kwa uovu wako, hilo ni jambo zuri! Kimbia kwake. Piga magoti kwa unyenyekevu na umshukuru kwa kukuonyesha ukweli kuhusu wewe binafsi. Ni uthibitisho kwamba Yesu anakufuata kwa upendo.

Acha uovu wako, na badala yake umgeukie Yesu. Jizike mwenyewe katika Biblia. Jijumuishe katika maombi. Tafakari juu ya, Yesu ni nani, na anaahidi kufanya nini ndani yako na kupitia kwako? Jinyenyekeze kwake ili uweze kumpendeza na kuishi kwa urafiki wa karibu naye. Kumbuka kwamba upendo na ahadi zake ndizo zinazokupa nguvu na mamlaka ya kuishi maisha safi.

Huu ni mchakato wa kila siku. Pale unaposhindwa, usinaswe na hatia au hisia ya kutokuwa na tumaini. Wakati unaposhindwa ndio wakati unahitaji kumgeukia Mungu zaidi. Wazo la kwamba uovu wako una nguvu zaidi kuliko Mungu ni la kijinga na kiburi. Yesu alikupenda ulipoishi kinyume naye, bila shaka atakusamehe sasa, wewe ni mtoto wake! Yeye ni mwenye nguvu zaidi kuliko uovu wako, na anakupenda zaidi kuliko wewe unavyojichukia. Amini hilo na hutapoteza matumaini.

Chimbua Kwa Kina

Soma 1 Yohana ya 1, Waefeso wa 5:8, na Yohana ya 11:9-10, kisha uandike uelewa wako wa msamaha na maana ya “kutembea katika nuru.” Sali kuhusu hilo, kisha jadili kwa unyoofu na rafiki Mkristo unayemwamini. Je, unatembea kwenye nuru? Ikiwa sivyo, ni mabadiliko gani unaweza kufanya leo ili kuingia kwenye nuru?